New (Audio) GK Feat Vanessa Mdee, Rawdgers & Hoox – Shukrani

New Track kutoka kwa Member wa iliyokuwa East Coast Team toka Upanga, King Crazy GK amevunja ukimya kwa kuachia ngoma mpya ambayo amewashirikisha Venessa Mdee, Rawdgers na J-Hoox inayokwenda kwa Jina la Shukrani. Ngoma hii imetoka Juzi baada ya Kimya Kirefu toka kwa Mkongwe huyu na Imefanywa chini ya Uangalizi wa Producer John Mahundi.
GK

Ukitaka kuisikia/Kuipakua Bofya hii link hapa chini.
https://www.hulkshare.com/ngomanagwa/gk-ft-vanessa-mdee-rawdgers-hoox-shukran

“New”(Audio) Dullayo Feat Prof Jay – Moko Moko

Mwanamuziki anayewakilisha Mziki wa Kizazi kipya ndani “Dullayo”, amekuja na Ngoma Mpya akimshirikisha Mkongwe “Prof Jay” na Track iliyopewa jina la “Moko moko” Ngoma hii imefanywa katika Studio za Mwanalizombe chini ya Producer Mashuhuri “Villy” Enjoy ngoma hii na Tutoe support kwa wasanii wetu wa Miziki ya aina Zote ndani ya Bongo. Bofya hii link Kuisikia na Kuipakua ngoma hii. http://hu.lk/ssv83s6lev40 Dullayo Feat Prof Jay

NEW Geez Mabovu Tribute Mix “Nov 2014” (C) Ngomanagwa

Geez Mabovu Tribute Mix

“Big 4 the Geez” ukipenda Unaweza Kumuita “Mwanamadharau” ama wengi walimuita “Geez Mabovu Jina kamili “Ahmed Ally Utepe” alikuwa ni Msanii wa Kizazi kipya aliyefanya mziki wa hip hop toka “Dirty South” Iringa, Tanzania. Geez alifariki dunia siku ya Tarehe 12 Mwezi wa 11 Mwaka huu baada ya kuumwa kwa muda mrefu. Wakati wa uhai wake alikuwa ni kati ya wasanii wachache ambao waliitendea haki Hip hop nchini Tanzania. Haukujalisha Mziki huu ulimlipa kiasi gani katika soko la Muziki wa kizazi kipya nje na ndani ya Bongo, Mchizi aligangamaa na kuendelea kufanya kazi yake ya Sanaa tokana na Mapenzi ya sanaa na kazi yake. Mtoto huyu wa kiume hakuyumbishwa tokana na air-time rediaoni ama kuandikwa mara kwa mara katika blogs ama kutangazwa na vyombo vya habari kwa nia ya kumpatia kipato zaidi, alipiga moyo konde ingawa ilikuwa ni ngumu ila hakufa moyo. Alikuwa na Urafiki wa karibu na wasanii toka Chemba Squad pia wasanii kadhaa toka Arachuga A-town city. Mimi pia nilikuwa ni shabiki mkubwa wa kazi zake na nilivutiwa zaidi na Style yake ya Kughani pamoja na sauti yake nzito ukilinganisha na umbo lake, pia mashairi yake ambayo yalikuwa ni ya kitaa zaidi yalikuwa yamesheheni aliweza ujumbe ulioeleweka kirahisi pindi ukimtegea sikio. Siku 3 baada ya Kifo chake nilipokea Maombi mengi toka kwa washabiki wake wakiniomba nifanye (Non-Stop) Mix ambayo itaenzi mziki wa GEEZ MABOVU nami sikufanya ajizi. Basi kama wewe ni Mshabiki wake wa kweli na ungependa kuendelea kumkumbuka Fanya kubofya link hii hapa chini usikilize/uipakue Mix hii Bure kama kumbukumbu ya kazi za Geez. #ForTheLoveOfHiphop #GeezMabovuTributeMix #RIPDirtySouthDawg

https://www.hulkshare.com/ngomanagwa/geez-mabovu-aka-mwanamadharau-tribute-mix-nov-2014-ngomanagwa

NEW (Audio) Jcb Feat Hisia – Mtoto Mkali

JCB_mtotoMkali

Mashabiki wote wa Bongo Hip hop, hii ni zawadi mpya toka kwa The GENERAL himself, toka katika Kundi la watengwa. This time amekuja na GHETTO LOVE joint, ambayo itakufanya moyo wako ukusisimuke. JCB ameachia “Mtoto Mkali” leo Rasmi kwa wana wote na wapenzi wa Hip hop baada ya muda kidogo maana yupo mbio na shughuli zake za maisha. Ngoma ni kali, Support Bongo Hip hop kama wewe ni mpenzi wa kweli wa huu mziki. Click link hii kuweza kuisikia/Kuipakua, Enjoy.

https://www.hulkshare.com/94woizjq40e8